26 Julai 2025 - 21:56
Zaidi ya Watu 10,000 Wanufaika na Huduma za Afya za Khoja Shia Ithnasheri Jamaat – Mwenyekiti Dewji Afichua Mafanikio

Khoja Shia Ithnasheri Jamaat Nchini Tanzania imeendeleza Utaratibu wake wa kutoa Huduma za Afya kwa Maelfu. Dewji ametoa Takwimu Kamili juu ya hilo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Alhaj Mohamedraza Dewji Mwenyekiti wa Taasisi ya Khoja Shia Ithnasheri Jamaat akiwa katika Mahojiano ya Uislamu na Jamii leo hii, Julai 26, 2025 kupitia IBN TV Africa ametoa takwimu muhimu kuhusiana na Huduma za Macho kwa watu wenye matatizo ya macho. Amesema:

"Mwaka jana tulikuwa na watu zaidi 10,000 na watu 8818 walipima macho, operesheni za mtoto wa jicho ni 510, dawa ya macho zilitolewa 2945, Miwani 2469, Damu Salama zilikusanywa  Pointi 281 kwa siku 3 zinasaidia katika hospitali kama Muhimbili"

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha